Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

WASANII WA BONGO MOVIES WAMPINGA WEMA SEPETU

$
0
0
Wasanii wa Bongo Movies waliokuwa wakishiriki kwenye kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ya Mama Ongea na Mwanao ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamezungumza na waandishi wa habari na kutoa msimamo wao kuhusu madai yaliyotolewa na mwanadada Wema Sepetu, kwamba wanakidai chama hicho fedha zao.

Wakizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Protea, wasanii hao wakiongozwa na Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ na Ndumbangwe Misayo ‘Thea’, wamesema madai aliyoyatoa Wema Sepetu hayana ukweli wowote kwa sababu wasanii wote walilipwa na Wema alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakiwalipa wasanii hao.
Mara baada ya Thea na Yobnesh kuzungumza maneno machache, mkutano huo na waandishi wa habari ulimalizika, ukiwa umechukua dakika chache tu na kuacha kila mtu akaizungumza lake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>