Naibu Katibu Mkuu CCM_Bara Mh:Mwigulu Nchemba akimnadi Mgombe wa Ubunge Jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete hii leo wakati wa Mkutano wa Hadhara wa Kampeni za Lala Salama Kata ya Pera.Uchaguzi Unategemewa Kufanyikwa Tar.06/04/2014 kumpata Mbunge wa Jimbo hilo,CUF na CHADEMA pia Wamesimamisha Wagombea kwenye Kinyang'anyiro hicho cha Ubunge.Ushindi ni Umoja,Mh:Mwigulu Nchemba ambaye amekuwa akiongoza Kampeni mbalimbali,Hapa akiwa na Mbunge wa Kalenga Godfrey Mgimwa na Mbunge Mtarajiwa wa Chalinze Ridhiwani Kikwete.Wameshikana Mikono kuamaanisha "UMOJA NI USHINDI""Tumewamaliza"
Mke wa Mgombe Mama Ridhiwani akimnadi Mme Wake Kwenye Kampeni za
Ubunge Jimbo la Chalinze.Kada wa Chama Cha Mapinduzi Husein Bashe akisikiliza Mkutano wa Kampeni hapa Pera.
Mbunge wa Kalenga Mh:Godfrey Mgimwa akimnadi Ridhiwani Kikwete na Kuwasisitiza Wananchi kuendelea Kuwaunga Mkono Vijana kwenye Nafasi za Uongozi.Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi Mtela Mwampamba akiwakwenye Mambo Poa ya CCM.
Mh:Nyalandu akiwasisitiza Wananchi Kufanya Maamuzi mema kwa Kumchagua Ridhiwani Kikwete,Mbali na Kampeni,Mh:Nyalandu amewaomba watanzania Kuendelea Kumuunga Mkono kwenye Vita Dhidi ya Majangili wanaoua Tembo na Faru.Ni Vita Ngumu inayohitaji Mshikamano Mkubwa sana.
Mh:Nyalandu akibadilishana Mawazo na Mke wa Ridhiwani Kikwete mara baada ya Kumuombea Kura Ridhiwani kwa Wananchi wa Pera.
Karibu Sana Mjengoni Dodoma,Mh:Nyalandu akisalimiana na Mbunge wa Kalenga Mh:Godfrey Mgimwa.
Mh:Nyalandu akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba
Katibu wa NEC Uenezi,Nape Moses Nnauye akiwahakikishia Wananchi kuwa Katibu wa Vijana yupo Kalinze kuhakikisha Uchaguzi unakwenda Salama hadi Mwisho.
Katibu Mkuu Jumuia ya Vijana(UVCCM) Mh:Sixtus Mapunda akiwahakikishia Wananchi uwepo wa Amani kwenye Zoezi Zima la Upigaji Kura.
Katibu wa Mkoa wa Mtwara CCM Ndugu Akwilombe akizungumza na Wananchi wa Kata ya Pera.Katibu huyu Wa Mtwara amewasihi Wanachalinze Kuchagua Kweli na Sio Uongo.Akwilombe amepuuza Vikali kuwa Watoto wa Viongozi wanabebwa kwenye Siasa,Amerejea kuwa Wale wanaosema hayo wao Ndugu,Kaka,Wajomba na Wake zao wamepea Ubunge na Nafasi za Uongozi ndani ya Vyama Vyao tena kwa Mabavu.Akwilombe amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa na baadae Kuhamia CCM.Kada Mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi na aliyewahi Kuwa Mwenyekiti wa Yanga Ndugu David Mosha akiwa Kwenye Mkutano wa hadhara wa Rafiki Yake Ridhiwani Kikwete hii leo Kipera.
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Mamia ya Wananchi wa Kata ya Pera waliojitokeza Kwenye Mkutano wa Hadhara wa Kampeni wa Chama cha Mapinduzi hii leo Chalinze,
Mgombea Wa Ubunge Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Kalenga Mh:Godfrey Mgimwa.
"Mambo Poa,Jiandae Kushinda kwa Kishindo" Mwigulu Nchemba.
Rafiki wa Ridhiwani Kikwete akipata Picha ya Kumbukumbu kwenye Mkutano wa Pera hii leo Chalinze.Vijana wakitoa Burudani ipasavyo kwenye Mkutano wa Kampeni Kata ya Pera hii leo.
Makada Watiifu wa Chama Cha Mapinduzi,Kushoto ni Emmanuel Shilatu na Anayefuatia nia Majura.
Hakika Ridhiwani Kwa Maendeleo ya Chalinze,Kijana wa CCM akiwa amevaa Bango lenye Ujumbe Kuhusu Chalinze na Kampeni za Uchaguzi Unaoendelea hasa kwa Chama cha Mapinduzi
Picha/Maelezo na Sanga Festo