Mamba aliekua akiishi katika ziwa Victoria mwenye umri wa miaka 80, mwenye uzito
unaokadiriwa kukaribia tani moja amekamatwa katika ziwa Victoria upande wa Uganda ni baada ya wananchi kulalamika kuhusu mamba huyo anaekula watu, huku akikadiriwa kuwa ameshakula watu wasiopungua sita mpaka kukamatwa kwake
watu wengi kutoka kijiji cha kakira walifika kushuhudia mamba huyo akitolewa majini, huku wakiwa na nyuso za furaha na wengi wakipiga picha
Mtu wa mwisho kuliwa na mamba huyo ni mzee mwenye watoto wawili ambae ni mvuvi wa samaki ambae nguo zake zilionekana zikielea katika mto huo huko Uganda.
source: BLOG YA VIJANA