PAMBANO la Kimataifa la Bondia, Francis Miyeyusho dhidi
Mfilipino Angelito Merin, limesogezwa mbele, ambapo sasa
litafanyika Jumamosi ijayo ya Aprili 12, kwenye Ukumbi wa (PTA),
Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam leo, mratibu wa pambano hilo,
Mussa Kova, alisema kuwa pambano hilo limesogezwa mbele,
ikiwa ni pamoja na hata kubadilisha bondia kutokana na kuna
watu wamewamehuju pambano lao.
Kova alisema kuwa pambano ilo ambalo lilikuwa lifanyike leo,
kufanya mpinzani.
Alisema licha ya kupanda Miyeyusho litakuwa la WBC, ambalo
litasimamiwa na PST, kutakuwa na pambano lingine la la
Kimataifa, ambalo litamkutanisha bondia Francis Cheka dhidi ya
Gavad Zohrevand kutoka nchini Iran.
Kova alisema pambano hilo la cheka ambalo litakuwa na raundi 6,
ambalo litakuwa la utangulizi, huku pambano lingine la ubingwa
wa Taifa litakuwa kati ya Cosmas Cheka dhidi ya Ibrahim Mawe,
ambapo pambano hilo litakuwa la raundi 10.
Alisema kitendo cha baadhi ya wadau wa ngumi kutuma ujumbe
kwenye mtandao, kimefanya pambano hilo kusogezwa mbele
huku wakibadilisha bondia, kutokana na bondia Ronald Pontillas.
Kova hata hivyo wamejipanga kumchukulia hatua kali, aliyehusika
kufanya hivyo ili iwe fundisho kwa wengine.
"Nimesikitishwa sana na kitendo hiki, lakini tuymeshajua nani
anayefanya hivi, ila ni lazima tumshukulie hatua ili iwe fundisho
kwa wengine, ametufanyia kitu cha ajabu sana"alisema Kova.
Naye Bondia Cheka, alisema kuwa yeye amuamua kupigana
pambano la kirafiki kwa kuwa anaona ni siku nyingi ajapigana,
kwa kuwa mpinzani wake ameumia mguu.
Cheka alisema hivyo kukaa kwake bila ya pambano, kunazidi
kumnyima hata, hela kwa kuwa yeye kazi yake ni kupata
mapambano ya ngumi.
"Nikikaa bila ya kupambana nakosa hela, hivyo ni bora nipigane ili
iweze kupata hela kwa sababu ngumi ndiyo maisha yangu"alisema
Cheka.
Pia Cheka alisema inasikitisha kuna baadhi ya viongozi wa vyama
wanaamua kuwaaribia mabondia wakipata pambano.
Alisema hata kuvurugika kwa pambano hilo kumesababishwa na
mmoja wa viongozi wenye kampuni za kuandaa mapambano ya
ngumi, ambaye anapenda watu waandae ngumi kupitia kampuni
yake.
Cheka alisema kitendo hicho kimefanya kidumaze mabondia kwa
sababu hawapati mapambano.
"Nashangaa viongozi wanaongoza vyama baada ya kutusaidia sie,
wanazuhia mapambano ya kimataifa yasifanyike"alisema Cheka.
mwisho