Wewe kama mtumishi wa Mungu hukutakiwa kuandika barua ikulu kwa sababu zifuatazo
kwanza kabisa kama mtumishi wa Mungu mzoefu ulitakiwa kukaa chini na kufikiri kabla ya kuandika
Pili unamuandikia barua mtu Ambae mna Imani tofauti katika kufanya kazi zake
tatu unajaribu kupigana vita ya kimwili wakati watumishi wa Mungu mnatakiwa kupigana vita ya kiroho
wewe ni Mtumishi wa Mungu wa muda mrefu sana,tangu nakua nasikia jina Kakabe,umekosea sana na imetokana na kiburi chako cha kutomshirikisha Mungu
ulitakiwa kufanya nini?
ulitakiwa kuongea na Mungu kama kweli wewe ni mtumishi wa Mungu
una uwezo mkubwa sana hapa duniani kuliko Kikwete na waliomzunguka
umeshindwa kujitambua kwamba una mamlaka wala huitaji kujiingiza kwenye upuuzi
una uwezo wa kukamata nguvu za giza anazotumia Kikwete wa wajinga wenzake kupitia ulimwengu wa Rohoukifunga na kuomba na kumweka Kikwete mbele za Mungu ungeona matokeo. - By Mdau