NYOTA wa sinema za Bongo, Wastara Juma ameibuka na kusema kuwa, kuna mwanaume asiyependa mafanikio yake kiasi kwamba alifurahia alipopata ajali na kuvunjika mguu, mumewe Juma Kilowoko ‘Sajuki’ kufariki dunia na akatangaza kwamba, mwanaume yeyote atakayemuoa atakufa kama Sajuki.
Katika mahojiano maalum na paparazi, Wastara alisema mwanaume huyo aliwahi kuwa nudakua uhusiano naye wa kimapenzi miaka ya nyuma, wakamwagana.
Wastara aliyasema hayo baada ya kupigwa swali kwamba, kuna madai kifo cha mumewe, marehemu Sajuki kilikuwa na mkono wa mwanaume aliyewahi kuwa mpenzi wake (jina tunalishikilia kwa sasa).
“Ni kweli kuna mwanaume niliwahi kuwa na uhusiano naye, alitangaza kwamba yeyote atakayenioa atakufa kama aliyokufa Sajuki.
“Ukiachana na Sajuki, nilipopata ajali mwaka 2009 nikavunjika mguu na kukatwa, huyo mwanaume ambaye tulishaachana siku nyingi, alitangaza kwa watu kwamba yeye alitaka nivunjike miguu na mikono yote ili niwe kama boksi,” alisema Wastara huku akilengwa na machozi.
paparazi: Sasa Wastara, kama hali ni hiyo wewe ulichukua uamuzi gani?
paparazi: Sasa Wastara, kama hali ni hiyo wewe ulichukua uamuzi gani?
Wastara: Nilikwenda kumripoti Kituo cha Polisi Oysterbay (jijini Dar).
paparazi: Okay, lakini unaonaje madai kwamba, huyo mtu anahusika na kifo cha Sajuki?
Wastara: Kusema kweli mimi siwezi kujua maana Sajuki aliumwa namuona, akazidiwa ikafika mahali Mungu akamchukua. Sasa kama ni mkono wa huyo mwanaume sijui ila ilivuma hivyo.

paparazi: Lakini kwa tangazo lake hilo, wewe umejipangaje? Maana wanaume watakuwa wanakuogopa!
Wastara: Kama yeye amejipanga iwe hivyo, hata mimi nimejipanga pia. Sina wasiwasi, lakini namtangaza huyo mwanaume kama adui yangu namba moja. Sina wasiwasi, siwezi kudhurika na wala mwanaume atakayenioa hawezi kudhurika.
Hayo ni maneno yake, akae nayo tu. Kama anataka vita, nipo tayari lakini siku zote mimi ni mkimya ila mtu akinikorofisha huwa nacharuka hasa.
paparazi: Tangu mmeachana na huyo mwanaume umewahi kukutana naye popote?
Wastara: Sikumbuki kwa kweli. Nadhani sijawahi kumwona ila yupo. Amekuwa adui hata wa familia ya kwetu kwa ajili ya matamshi yake hayo.
Wastara: Sikumbuki kwa kweli. Nadhani sijawahi kumwona ila yupo. Amekuwa adui hata wa familia ya kwetu kwa ajili ya matamshi yake hayo.
paparazi: Kwani kuachana kwenu kulitokana na nani?
Wastara: Mimi nilimchoka kwa tabia yake. Alikuwa hajatulia. Mbaya zaidi manyanyaso yalikuwa kila siku. Sijawahi kufurahia uhusiano wangu na yeye.
Wastara: Mimi nilimchoka kwa tabia yake. Alikuwa hajatulia. Mbaya zaidi manyanyaso yalikuwa kila siku. Sijawahi kufurahia uhusiano wangu na yeye.