STAA asiyekaukiwa habari Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa ‘anainjoi’ kuona mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ anamuonea wivu kwani anaamini ndiyo penzi la dhati.
Akifafanua hilo mbele ya kinasa sauti chetu, Wema alisema wivu kwake ni kipimo kikubwa cha kutambua Diamond anamzimikia kiasi gani.
“Baby (Diamond) anavyonionea wivu mimi ndiyo ananichanganya kabisa, najisikia faraja maana angekuwa hanionei wivu ningejua wazi sipendwi,” alisema Madam.