BAADA ya Mshambuliaji wa Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mrisho Ngassa kukana kuwa hana mahusiano na msanii wa muziki wa kizazi kipya Snura huku Snura pia akifafanua kuwahawana mahusiano ya mapenzi, mshambuliaji huyo hivi sasa amehamishia majeshi yake kwa msanii wa filamu nchini Wema Abrahami Sepetu ambaye pia amewahi kuwa miss Tanzania. Ngassa ameingia katika rekodi ya wachezaji wa Bongo kuzama kwenye mapenzi na wasanii maarufu wa filamu nchini.Baadhi ya
![Mrisho Ngassa alivyo kuwa katika mahaba mazito na Snura,akisuka nywele za mpenzi wake.](http://www.habarimpya.com/images/Ngassa%20msusi%20wa%20snura450pixel%20size.jpg)
wachezaji waliowahi kuzama katika mapenzi ya wasanii wa filani kiasi cha kuhatarisha hata viwango vyao ni pamoja na Kipre Tchetche aliyewahi kuzama kwenye penzi la Jackline Wolper, huku wakigombea penzi la msanii huyo yeye pamoja na mdogo wake Michael Baluu kwa nyakati tofauti.
Kama ilivyo kwa Irine Uwoya aliyewai kuzama kwenye penzi lamwanasoka Hamad Ndikumana kutoka Rwanda kiasi cha kufunga ndoa na kuzaa mtoto mmoja.
Hata hivyo ndoa ya mwanadada huyo nyota wa filamu ilivunjika miaka miwili iliyopita baada ya kugoma kwenda kuishi nchini Rwanda ambako ndipo kwao na mwanasoka huyo.
Taarifa za ndani zilizonaswa na Habarimpya.com zinaeleza kwambwa Ngassa ameanza kuzama kwenye penzi la Wema Sepetu baada ya kuzoeana na msanii wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kwa jina la 'Diamond'.
Watu wa karibu na mwanasoka huyo mwenye visa vya mapenzi kuliko wote nchini wanafafanua kwamba Ngassa ameanza kuwekeza maisha yake kwa Wema bila kujali bifu linalofukuta kati yake na Diamond.
"Ngassa na Wema wana mahusiano mazito ingawa mahusiano yao si ya muda mrefu sana lakini katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakiyanogesha huku kila mmoja akiyafanya kuwa siri, ingawa kazi kubwa iko kwa Ngassa kwa sababu mwenzake amezoea mikiki ya kuanika mahusiano yake lakini jamaa anaogopa na hapendi kabisa kitu kama hicho kijulikane"alisema mtoa taarifa wetu jina limehifadhiwa kwa sababu za kiusalama.
Source:Habarimpya.com