Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

SUPER STAR JUMA NATURE AMFUNGUKIA JOKATE MWEGELO KIDOTI ONA HAPA ALICHOSEMA LIVE!!

$
0
0

JUMA NATURE ASEMA JOKATE KAMUIGA KUANZISHA BIASHARA YA NDALA



Chelewa chelewa, utakuta mwana sio wako!! Ndicho kilichotokea kwa Juma Nature ambaye wazo lake la kuanzisha ndala liliendelea kuwa la mdomoni na ‘kutalk the talk’ ilhali Jokate Mwegelo akileta action kweli kwa ‘kuwalk the walk’. Baada ya mwanamitindo na mtangazaji Jokate Mwegelo kuanzisha ndala zake kupitia brand yake ya Kidoti, Juma Nature ambaye nae alikuwa na wazo hilo kwa muda mrefu, amefunguka na kusema Jokate amemgeza.
Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM leo,Juma Nature amesema kuwa ingawa Jokate ametoa tayari ndala zake, naye pia ataingiza sokoni brand yake.
“Nani katoa we?”, alihoji Juma Nature aliyeonekana kutokuwa na habari hiyo. “Najua si msanii mwenzangu lakini inakuwaje! kama ametoa itakuwa ameiga nanihii yangu mimi fresh tu,mwache zimsaidie maisha, si idea yangu hiyo! Kutoa ni lazima nitoe kwasababu mimi naitwa Nature,Nature ni yule yule wa miaka na miaka,hatopotea hata kidogo. Mimi bado kidogo kwasababu na mambo mengi sasa hivi nafanya katikati hapa nadhani mashabiki wangu wakitaka kujua waangalie katika TV. Nadhani kila mtu anajua kwasababu gani? Hakuna msanii ambaye alishawahi kutangaza kwamba anategengeneza project ya ndala zaidi yangu.”chanzo Bongo 5

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>