Marehemu Catherine Mhlaba, 45 |
Mwanamke anyejulikana kwa jina la Catherine Mhlaba mwenye umri wa miaka 45 raia wa Zimbabwe amejiua kwa kujichoma moto pamoja na mwanae ambaye alikuwa Disabled.
Habari zinasema mwanamke huyo alifikia hatua sababu ya mapenzi. Bwana aliye kuwa nae alimuacha akachukua mwanamke mwingine hapo hapo karibu na kwake akaona hawezi vumilia.
Habari zinaendela kudai kwamba juzi kabla ya tukio aliwatumia ndugu zake ujumbe wa SMS na kuwaeleza kwamba anaenda kujiua na baada ya hapo akazima simu yake na ndipo alimchukua mwane huyo wakaingia kwenye gari na kuelekea maeneo ambayo yandaiwa huyo mwanaume alikuwa akiisha na huyo mwanamke wake mpya.
Gari aliyokuwemo Catherine na mwanae ikiwaka moto |
Baada ya kufika maeneo hayo ambayo ni karibu na bahari habari zinaendela kudai kwamba gari lilionekana lilionekana linasogea mbele na baada ya kama dakika moto mkubwa ulilipuka kutoka kwenye gari.
Inadhaniwa alimwaga petrol kisha akawasha moto. Zimamoto walifika eneo la tukio na kufanya juhudi zote lakini hawakuweza kuwaokoa na ilichukua zaidi ya nusu saa kuuzima moto huo. Police walipo fika wakakuta mwili wa Catherine na mwane wakiwa wamesha kufa ndani ya gari.