MASKINI! Msanii wa filamu Bongo, Lungi Maulanga amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya gari na kupata majeraha mbalimbali mwilini.
Lungi alipata ajali hiyo maeneo ya Tegeta, jijini Dar akiwa kwenye gari lake ambapo aligongwa na lori lililokuwa limebeba mchanga na kusababisha aumie zaidi usoni na mguuni na kushonwa nyuzi tisa. “Namshukuru Mungu nimeponea chupuchupu kwani lori lilikuwa linakuja kwa kasi mbele yangu ambapo ilikuwa tukutane uso kwa uso nikakimbilia pembeni ndipo likanigonga kwa pembeni,” alisema Lungi.