Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba tunaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) tumefanya uamuzi wa hekima na busara wa kuondoka kwenye Bunge la Katiba baada ya kutoridhishwa na mambo yafuatayo:
1. CCM kupindua Rasimu ya Katiba ya Wananchi na kupenyeza Rasimu yao yenye lengo la kuwalinda watawala na mafisadi.
2. Waziri William Lukuvi kutumia Kanisa kupandikiza chuki na kuchochea vurugu kwa kurejea kauli ya Rais Jakaya Kikwete kwamba ukipitishwa muundo wa Muungano wa Shirikisho la Serikali Tatu, jeshi litachukua madaraka na kwamba Zanzibar itaunda Dola ya Kiislamu dhidi ya Wakristo.
3. Mjadala wa Bunge la Katiba kugeuzwa jukwaa la kuhubiri matusi, chuki, ubaguzi wa rangi na ukabila.
Tunawaomba wananchi watulie na wasubiri kauli za viongozi wao juu. Wasiwe na khofu. Kwa kupitia njia za amani na demokrasia, Katiba ya Wananchi itapatikana.
Na Ismai Jussa Facebook