Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

HABARI YA MUJINI SKYLIGHT BAND WATIBITISHA HABARI ZA KIFO CHA MWANAMUZIKI WAO MAARUFU!!

$
0
0
10173726_10152036323227864_1413106576404088176_n
Mpiga Gitaa wa Skylight Band maarufu kwa jina la Chiri Challa(pichani) amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia April 17 katika Hospitali ya Muhimbili.

Taarifa za awali zimethibitishwa na uogonzi wa bendi hiyo kuwa mpiga gitaa huyo machachari amefariki baada ya kuugua kwa siku mbili ugonjwa wa kupooza nusu ya mwili wake na kuepelekea kutofanya kazi ipasavyo.
Kwa mujibu wa Meneja wa bendi hiyo  Aneth Kushaba AK47 Ugonjwa wa kupooza ulipelekea mishipa ya damu kichwani kupasuka hivyo na kumsababishia maumivu makali  sehemu kichwani.
10268531_10152035773597864_7736400417218686840_n
Kutokana na msiba huo uongozi unapenda kutoa taarifa kuwa Show ya Escape One iliyokuwa ifanyike Alhamis ya April 17 imeahirishwa hata hivyo uongozi unasikitika kumpoteza msanii huyo ambaye alikuwa ni kiungo muhimu wa bendi na inaungana na familia ya marehemu Chiri Challa kuomboleza kifo cha mpendwa wao na inatoa pole kwa familia na mashabiki wa Skylight Band na wapo bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.
Msiba na shughuli za mazishi zinafanyika maeneo ya Mwanyamala Ujiji mtaa wa Mpunga.
Kwa mawasiliano zaidi namba ya Meneja wa Bendi +255  715 677 499.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>