Apr 20, 2014
Na Francis Godwin, Iringa
ASKOFU mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya Iringa Dkt. OwdenburgMdegela ameitumia ibada ya Jumapili ya Pasaka leo kulaani vikali wale wote wanaowatukana waasisi wa Taifa hili Sheikh Abeid Amani Karume na Mwalimu hayati Julius Kambarage Nyerere.
Askofu Dkt Mdegela amesema kuwa watu hao wanapaswa kuwaomba radhi watanzania huku akisisitiza wajumbe umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kurejea bungeni ama kufungasha virago vyao na kurudi nyumbani kwao na sio kuzunguka kupandikiza chuki kwa wananchi.
Askofu Dr Mdegela, ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, aliyasema hayo leo wakati akitoa salam za pasaka kwa waumini wa Dayosisi hiyo kupita washarika wa kanisa kuu.
Dkt. Mdegela asema “Watanzania tunataka kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani na kuanza kutafuta kuvuruga amani na utulivu wetu ambayo ni lulu ya pekee inayogombewa na nchi nyingine na kuwa wanaotaka lulu hiyo ivurugike wasivumiliwe kamwe.
“Kinachofanywa bungeni kwa sasa ni mzaha wa hali ya juu na Watanzania wanapaswa kuwachunguza vema wawakilishi wao hao wakiwemo wabunge wa vyama vyote na wale wanaoeneza mbegu ya chuki wasichaguliwe tena….”
Asema wajumbe wa bunge la katiba hawana sifa ya kutengeneza katiba kwani wametanguliza mzaha na matusi yasiyo na tija na kuwa hawa wanaokwepa bunge na kutaka kuzunguka kwa wananchi wanapaswa kuzuiwa kufanya hivyo na vyombo vya usalama kwani wanataka kuipeleka nchi pabaya.
“Kama wamekula pesa za wananchi kwa muda wote huo kwa ajili ya kuunda katiba iweje leo watoke bungeni na kudai kuja kwa wananchi mikono mitupu??” amehoji.
“Wananchi tuwakatae wajumbe wanaotaka kuzunguka kupandikiza chuki kwa wananchi kwa kujiita wao wapo kwa ajili ya katiba ya wananchi hali wamekimbia bunge na kutaka kutuwakilisha nje ya bunge
“….tunawakataa wao na mawazo yao na pia kama wajumbe wa bunge hilo wameshindwa kazi tutaikataa rasmu ya katiba ambayo italenga kutugawa watanzania.
“Na niweke wazi mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba mbali ya kazi hiyo bado tunawajibu wa kumrekebisha pale alipokosea kwani Wazanzibar wa Pemba wanataka serikali nne sio tatu mbona hajaeleza
” ….nasema serikali mbili ni jibu kama haiwezekani bado tuwe na serikali moja itakayotuunganisha”
Hata hivyo Dr Mdegela alisema kuwa msimamo wake na waumini wa kanisa hilo ni kuwa na serikali mbili na ikiwezekana kuwa na serikali moja pekee na si vinginevyo na iwapo wajumbe wa bunge la katiba wameshindwa kazi na kugeuza bunge hilo ni sehemu ya kuonyeshana ujuzi wa kutukanana ni vema wakirudi katika mwelekeo mzuri ama kurudi majumbani kwao ili viongozi wa dini mashekhe na maaskofu wakaifanya kazi hiyo ya kuunda katiba bila kutukanana .
“Nimejizuia sana kwa kipindi hiki cha bunge la katiba nisiseme chochote ila kutokana na mambo jinsi yanavyokwenda uvumilifu umenishinda nimelazimika kusema na ninachosema nimekiandika ili wale wapotoshaji washindwe kupotosha ninachosema….wayahudi walikataa kuongozwa na Samweli kwa sababu walisema watoto wa Samweli wanatabia mbaya …walikataa kuongozwa na Mungu kwa madai kuwa na wao wanataka mfalme wetu uli tukienda kupigana na watu ili tuwe kama mataifa mengine ila Mungu hakutaka wao kuwa kama mataifa mengine ila wao wanataka kuwa kama mataifa mengine ….Samweli akaenda mbele ya Mungu akilia ….ila Mungu akasema hawajakukataa wewe wamenikataa mimi …enyi watanzania tukikataa lulu tuliyopewa na Mungu ya kuwa nchi ya amani tutakuwa hakuwakatai viongozi wetu tutakuwa tunamkataa Mungu”
Aliwataka watanzania kuyatazama mataifa jirani kama Kenya ambao walijipenda wao na kushindwa kuwapenda majirani sasa Wasomari wameingia wanawasumbua ila tazameni pia Malawi ambao walimtaka rais wao awe Joys Banda ila alipoingia tu Ikulu alitangaza ndoa za jinsia moja pamoja na nchi ya Kongo ambayo imesaidiwa na Tanzania kurudi katika amani ikiwemo nchi ya Burundi ambayo Rais wake amekuwa akishinda katika maombi kwenye kanisa lake na kuacha kuongoza nchi.
“Tunapaswa kujiuliza amani hii iweje leo ichezewe na watu wachache wenye uchu wa madaraka na hata kususa bunge la katiba …hatujifunzi kutoka nchi za majirani zetu kama Uganda ,Rwanda kuna vyama 10 vya upinzani na kuna vikundi 10 vinavyotaka kumpindua Rais huku Uganda kuna mtu anaitwa Kony yeye siku zote kumshumbua Rais ….ninyi ni nani Tanzania bara na visiwani mkaa kwenye amani kiasi hiki na mnakataa umoja na kuanza kuwasikiliza wanaopandikiza mbegu ya kuvuruga amani ya kutaka serikali tatu ….watanzania tunataka kuikataa lulu tuliyopewa na Mungu lulu ya amani”
Dr Mdegela alisema kuwa hadi sasa mwenendo wa bunge la katiba unatia aibu kubwa kwa Taifa na hata nje ya taifa hili na kuwataka wajumbe hao kuwa wasikivu na kama walisema wanakwenda kuandaa katiba ya wananchi iweje kabla ya kuanza kwa bunge hilo walianza kwa kulilia posho kuongezwa hali wakijua walimu hawajalipwa malipo yao pamoja na wafanyakazi hawajaongezwa mishahara yao.
“Natamka wazi kuwa mimi Dr Mgedela sina imani hata kidogo na wajumbe wa bunge la katiba …..kama wanavyoonekana na walivyo wana hadhi ya kutoridhika watatuletea katiba mbovu kwa sasa na wao ni wabovu ..
“Natamka rasmi kuwa tume iliyoandaa rasmi ya katiba haukuandaa msaafu wala Biblia ili andaa kitu ambacho mbacho kinaweza kuhojika na kukataliwa ama kukubalika wao si Miungu ni wanadamu kama sisi madai kuwa wanavyeo vingi serikalini hata mfagiaji anavyo ….sasa naiomba serikali hao waliojitoa bungeni wanataka kuja kwa wananchi tunasema hatuwataki ….
“Hivi kama mtu ameshindwa kujenga hoja bungeni watakuja kutueleza nini nawaombeni usalama wa Taifa fanyini kazi ya kulinda amani yetu ….kama hawataki kurudi bungeni basi waende majumbani kwao”
Askofu Dr Mdegela alisema kanuni za bunge wametunga wao na iweje leo wanakimbia kanuni waliyoitunga hivyo kama wanaona kanuni ni mbaya basi watuombe Watanzania wenye akili tuwasaidie hata yeye anaweza kwani wajumbe hao ni walafi wasiopenda amani ya nchi hii.
Katika hatua nyingine askofu huyo alisema kwa sasa kinachoendelea na kuwa kila kanda itataka serikali yao iwapo hoja ya serikali tatu ikapitishwa.