Kuna vitu vingi ambavyo wanadamu tunakuwa hatuna uhakika navyo ambapo baadhi yake hupata uhakika wake wakati unapofika, na vingine hatupati uhakika wake kwa kipindi chote cha maisha yetu.Hali hii hutupelekea wakati mwingi kujikuta tukiishi maisha ya kushuku shuku tu!.Hata hivyo kwa sasa angalau watanzania tuna uhakika juu ya 'facts' zifuatazo;
FACT1:Kuwa Katiba ni tendo la kisiasa,hivyo uundaji wake lazima uhusishe michakto ya kisiasa.Angalau hli sasa tuna uhakika nalo.
FACT2: Kwamba Siasa za Tanzania kwa kiasi kikbwa zinafanywa katika mfumo wa vyama vya siasa. Angalau hili nalo tuna uhakika nalo.
FACT3: kwamba msingi moja mkubwa wa demokrasia ni wengi wapewe (hata kama wanatetea jambo ambalo si zuri) na wachache wasikilizwe (hata kama wanatetea jambo lisilo zuri).Hilo nalo tuna uhakika nalo.(suala la kwamba semokrasia bado ni mfumo unaotufaa au laa! ni mjadala wa peke yake).
FACT 4: Kwamba kwa sasa wabunge wengi ni wa CCM, na wamepatikana kama matokeo ya mchakato wa kidemokrasia (hata kama mchakato huo ulikuwa na udhaifu wa hapa na pale ua hatufurahishi na hali hiyo) lakini angalau hili tuna uhakika nalo vile vile .
FACT5: Kwamba hakuna mtu ambaye yeye ni mwananchi zaidi ya wenzake; hata kama ana akili kubwa au ndogo kiasi gani. Hili nalo tuna uhakika nalo.
FACT 6: Kwamba mbunge anayeamua kwenda kinyume na misimamo ya chama chake, huonekana kama msaliti hata kama anatetea kitu kizuri kiasi gani.Hii ni kwa vyama vyote vikubwa tulivyonavyo kwa sasa (rejea kesi ya Himid {ccm} zitto {CHADEMA} Hamad Rashid {CUF} N.K} Angalau sasa tuna uhakika juu ya hili.
FACT 7: Kwamba vyama tulivyonavyo vinapenda kuwafanyia wengine (vyama vingine/wananchi wengine) yale ambayo wao hawataki kufanyiwa, na ndio maana Kwa mfano Zitto alipo simamia mambo ya msingi kabisa kinyume na uongozi wa chama chake, alionekana msalti (mfano mmoja miongoni mwa mingi); lakini wale wale waliomuona msaliti; wanataka zipigwe kura za siri ili baadhi ya wabunge wa CCM Waweze kwenda kinyume na msimamo wa chamo chao lakini kwa siri sana kwa kuchangia kitu kingine na kupigia kura kingine (kwa hoja ya kwamba watakuwa wanatetea kitu kizuri), na ndio maana wabunge wa CCM nao hushangilia msimamo wa chama chao hata kama wao hawana hoja za kuutetea kwa kuogopa kuhusishwa na usaliti.Angalau hili nalo sasa tuna uhakika nalo.
FACT 8; Kwamba wajumbe wote walioko bungeni ni wananchi na wanawakilisha wananchi wenzao bila kujali ubora wa mawazo waliyobeba.Kwa kuwa jamii wanayoiwakilisha ni “Heterogenious” vile vile tunategemea kwamba mawazo ya wawakilishi yatakuwa “hererogenius”vile vile , lakini utofauti wa mawazo hayo hauwezi kulifanya kundi moja/mjumbe mmoja kudhani ndiye anaewawakilisha na mwenye haki ya kuwawakisha wananchi zaidi wenzake.Kwa hiyo linapotokea kundi la wanasiasa likadai kwamba lenyewe ndilo linalowawakilisha wananchi zaidi ya wengine kwa kujipa mamlaka hayo lenyewe na kisha kuchukua hatua za kususia raratibu za kikanuni na kisheria; inakuwa si sahihi sana.
FACT 09: Kwa kuwa waliosusia bunge ni baadhi ya vyama vya siasa, bila shaka hii ni dhahiri kwamba watakuwa wamebeba ajenda za kivyama (suala la kwamba ajenda zao zitakuwa zinakubalika na wananchi wengi au laa ni mjadala mwingine).Laiti wangesusa kundi la 201, kungekuwa na hoja kwamba wanapinga hoja ya bunge kutekwa na vyama kwa kuwa wao hawatokani na vyama.Hili nalo sasa tuna uhakika nalo.
FACT 10: Kwamba katika siasa, upande mmoja unaposusa kushiriki; unatoa nafasi ya upande mwingine kushinda na kupitisha hoja , na kususia mjadala kwa hoja ya kwamba mwenzako hana hoja za maana, unamfanye asiye na hoja za maana kuonekana ndio wa maana kwa kuwa ndiye alietoa hoja na wewe ulisusa.
HITIMISHO:
Alieshauri juu ya mbinu ya kususasusa katika siasa za Tanzania kwa mazingira ya Tanzania amewainiza mkenge wenzake.Wanaofanya siasa za kususa wanaelekea kwenye“Tragedy of political miscalculations” kwa bahati mbaya au kwa kukusudia!. Hata kama wakiandamana; bado kikanuni , kisheria na kitaalam; maandamano hayawezi kutupa data za kisayansi kusukuma ajenda mbele.
Kwa kuwa ni kweli na tuna uhakika kwamba bado CCM ni wengi (hata kama hatupendi, au tunaamini haikutakiwa kuwa hivyo) jambo la kufanya ni kufikiri kwamba nini tunaweza kufanya tukaaminika na kupata uungwaji mkono na watanzania mara dufu ya wale ambao bado wanawaunga mkono CCM na hapo ndipo tutakapoweza kusukuma mbele agenda tunazodhani ni nzuri kwa kufuata kanuni za kidemokrasia.
N.B: Ikumbukwe kwamba hakuna hoja inayoweza kukubaliwa na watanzania wote wakati wowote hata iwe nzuri kiasi gani.
Mwandishi wa makala hii kaandika kama mchambuzi wa siasa na si kama mwanachama wa chama cha siasa.