Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MBURULAAAAAA AVUA NGUO ZOTE NA KUPANDA JUU YA NGUZO KUBWA YA UMEME

$
0
0

MTU mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Shija Machiya (30), mkazi wa Kijiji cha Butulwa, Kata ya Old Shinyanga alizua kizaazaa, baada ya kupanda kwenye nguzo ya umeme ya njia kuu inayopeleka umeme mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu wilayani Kahama.Machiya alipanda katika nguzo hiyo inayosafirisha umeme wa msongo wa KV 220 katika eneo la Ihapa jirani na Kiwanda cha Nyama na kusababisha taharuki kwa wakazi wa maeneo hayo.Tukio hilo lilitokea saa5 asubuhi, ambapo wakazi wa eneo hilo waliacha shughuli zao kwa muda wakifuatilia tukio hilo pamoja na kuhofia maisha mtu huyo.Mama mzazi wa Machiya, Mondesta Madirisha, alisema kuwa kwa
kipindi cha wiki moja mtoto wake huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kuchanganyikiwa akili.Alisema kuwa wanahisi kuwa tatizo hilo lilitokana na kuugua malaria ambapo waliamua kumpatia dawa za kienyeji na hali yake ilionyesha kuwa ni ya kuridhisha.“Tulipompa dawa ya kienyeji alipona kabisa, lakini jana tu kwenye mida ya saa mbili asubuhi, hali yake ilibadilika ghafla. Alianza kupiga kelele, akatoroka nyumbani na kuanza kukimbia ovyo barabarani, hali ambayo ilisababisha baadhi ya wananchi kuanza kumfuata,”alisema Madirisha na kuongeza:Bofya hapa inaendelea >>>>>>

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>