Maneno yalikuwa yanasemwa mtaani na baadae ikajulikana kuwa ni kweli Kajala na Wema hivi sasa wapo katika ugomvi mkubwa tu, jambo ambalo Kajala mwenyewe alifunguka kuwa, Ndio tunaugomvi kama walivyo marafiki wa kawaida kugombana, ila muda ukifika tutayamaliza”, hiyo ndio kauli ya kajala toka akiri kuwepo kwa ugomvi huo, huku kwa upande wa Wema mambo yako hivi;
“Thank you ma love for zawadi… hapa meno sasa kuoza ni lazima… I loooove looooove loooooove you… Raha ya kusafiri zawadi… God bless u ma love…@auntyezekiel@auntyezekiel@auntyezekiel@auntyezekiel@auntyezekiel Sasa basi najua nina deni la pictures… Hapa nafanya kazi ya kuzikusanya zooooote… Kesho mtachoka nyie… Maana ni tokea Mtwaraa si mnakumbuka…. Mi nawapenda sana…”aliyatumia Wema Sepetu maneno hayo kupitia uwanja wake wa kujidai wa instagram.
Wakati kajala akiwa bado amem-miss Best yake Wema Sepetu na kusubiri kwa hamu siku ile ifike waweze kusuluhisha tofauti zao, huku nyuma ushosti wa Wema na Mwigizaji mwenzie maarufu kama AutyEzekiel ndio kwanza unapamba moto, ukiwa una ambatana na kutumiana zawadi kama hizo hapo, ushostito wao huo umezidi kufana baada ya bifu hilo kati ya Wema na Kajala.