Ukiongelea moja ya mashindano yanayopeperusha bendera ya Tanzania nje ya nchi Tanzania basi Shindano la Miss Tanzania USA ni moja wapo, shindano hili lililo anzishwa na mwanamitindo Winny Casey linalohusisha warembo wakitanzania wanaoishi nchini Marekani. Mrembo anaeshikilia taji la Miss Tanzania USA, Joy Kalemere alilovishwa mwaka Jana 2013 anaendelea na ziara yake nchini Tanzania ilioanza leo Jumatano 5/7/2014 akitokea nchini Marekani akiongozana na mzinduzi wa shindano hili Ms Winny Casey.
Miss Tanzania USA, Joy Kalemere alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa Habari asubuhi ya Leo kuhusu ziara yake nchini Tanzania, huku akizungumzia zaidi nia yao ya kusaidia watoto yatima na pia kutangaza Tanzania. Mara baada ya mazungumzo na Waandishi wa Habari kamati ya Miss Tanzania USA ilielekea katika shule ya watoto yatima ya wanawake iliopo Mbezi Mwisho.
Wakiwa shuleni hapo walipokelewa kwa furaha na shangwe kutoka kwa wanafunzi hao huku wakikaribishwa na ngoma ilioandaliwa na wanafunzi wa shule hio, kisha Miss Tanzania USA Joy Kalemere aliweza kutoa hotuba kwa wanafunzi wa shule hio huku ndani ya hotuba hio akiwahamasisha wanafunzi hao ambao ni watoto yatima yasikate tamaa ila wazingatie ili kufikia malengo yao.
Wanafunzi walipata nafasi ya kumuuliza maswali mrembo Joy na kwa upendo mrembo huyo aliwajibu kadri ya uwezo wake huku nyuso za furaha na kuridhika zikionekana kwa wanafunzi hao kwa majibu waliokua wakipokea kutoka kwa mrembo Joy. Wanafunzi walipata nafasi ya kupiga picha na Mrembo Joy huku pia walipata nafasi ya kumuona mrembo Joy akitembea mwendo wa kiMiss live mara baada ya kumuomba afanye hivyo.
Kamati ya Miss Tanzania USA ikiongozwa na Ms Winny Casey waliweza kuwapatia vitabu wanafunzi hao kama zawadi kwao pamoja na CD ya shindano la Miss Tanznia USA 2013 lililo fanyika Marekani mwaka Jana.
Ziara ya Kamati ya Miss Tanzania USA nchini Tanzania inaendelea huku Miss Tanzania Joy Kalemere na Kamati nzima itafika jijini Arusha kwa muendelezo wa ziara yao katika moja ya shule iliopo jijini Arusha maeneo ya Monduli nje kidogo ya mjini.