Kikao muhimu sana cha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi akitoa maelezo juu ya maendeleo ya sekta ya nishati kwa Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ubou Sabaa (aliyeketi upande wa kulia). Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kuwasilisha taarifa ya maendeleo ya sekta ya nishati katika maeneo ya ulipaji kodi, mapato, ujenzi wa bomba la gesi ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa shirika la TANESCO. (picha: blogu ya Lukaza)
↧