MSANII mahiri wa komedi ambaye pia ni Mwimbaji wa Injili, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ amenaswa akichati kwenye simu wakati viongozi wa dini wakishusha maombi mazito.
Msanii mahiri wa komedi ambaye pia ni Mwimbaji wa Injili, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ akichati uku maombi yakiendelea
Tukio hilo lililowachefua baadhi ya waumini lilitokea hivi karibuni katika Uwanja wa Shule ya Msingi Saba Saba, mjini Moro ambapo Masanja aliyekuwa meza kuu, wakati wenzake wakiongoza sala ya kufungua kongamano hilo, yeye alikuwa bize na simu.
Kitendo hicho kilidumu kwa dakika kadhaa kisha staa huyo ambaye pia ana ndoto ya kuwa mchungaji mkubwa nchini, akajiunga na wachungaji wengine waliokuwa meza kuu kuendelea na sala.