Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
MAMIA ya wanachama wa Simba SC mchana wa leo walimsindikiza mwanachama mwenzao, Evans Elieza Aveva kwenda kuchukua fomu ya kugombea Urais wa klabu hiyo katika uchaguzi ujao Juni 29, mwaka huu.
Wanachama hao walimlaki Aveva barabara ya Lumumba na kumsindikiza kwa maandamano hadi makao makuu ya klabu, wakipitia barabara ya Uhuru na baadaye Msimbazi, yalipo makao makuu ya klabu yao.
Hata hivyo, wahusika wa makao makuu ya klabu walilazimika kuuzuia msafara huo na kumruhusu Aveva aingie na mtu mmoja tu kwenda kuchukua fomu, Saidi Tuliy, ambaye naye alichukua fomu ya kugombea Ujumbe.
Alipoingia alitoa kadi yake ya uanachama kujitambulisha kwa mtoa fomu, kisha kukabidhi ada na kupewa fomu yake kabla ya kuondoka kwa maandamano mazito.

Pointi tatu; Aveva akionyesha vidole vitatu wakati wa maandamano kumaanisha sera yake ni ushindi |
Mimi ndiye rais wenu; Aveva akiwaonyesha alama dole tupu wanachama wa SImba SC wakati wa maandamano |
Umati uliomsindikiza Aveva kuchukua fomu |
Aveva akionyesha kadi yake ya uanachama, kulia ni Said Tuliy |
Aveva akikabidhiwa fomu yake ya kugombe Urais |
Alipoingia alitoa kadi yake ya uanachama kujitambulisha kwa mtoa fomu, kisha kukabidhi ada na kupewa fomu yake kabla ya kuondoka kwa maandamano mazito.
Wakati wa maandamano wanachama walikuwa wakisukuma gari ya Aveva kuanzia Lumumba hadi makao makuu na mgombea huyo alikuwa akionyesha ishara ya vidole vitatu, akimaanisha sera yake ni pointi tatu- maana yake ushindi.
Na alipofika makao makuu wanachama ambao walikuwa hapo wakimsubiri nao walimlaki kwa shangwe, wakisema; “Huyu ndiye rais wetu,”.

Kwa ujumla mapokezi ya Aveva yanaweza kuwakatisha tamaa watu wengine kujitokeza kuwania nafasi hiyo, kwani Mwenyekiti huyo wa zamani wa Kamati ya Usajili ameonekana kuungwa mkono na watu wengi.
Ni mtu mmoja tu hadi sasa ambaye tayari amechukua fomu ya Urais mbali na Aveva, ambaye ni Andrew Tupa, lakini habari zinasema mwanachama mwingine maarufu wa klabu hiyo, Michael Richard Wambura naye atachukua fomu ya nafasi hiyo kesho.

Kihistoria Aveva ni Simba damu ambaye amekuwa akiisaidia klabu hiyo kwa zaidi ya miaka 20 sasa ni miongoni mwa waasisi wa kundi la Friends Of Simba (F.O.S.), ambalo limekuwa na msaada mkubwa wa kifedha katika klabu hiyo.
Hajawahi kuwa kiongozi wa kuchaguliwa, lakini amekwishaongoza kwa mafanikio Kamati kadhaa, ikiwemo ya Usajili mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambayo ilifanya kazi nzuri ya kuibua vipaji kama vya akina Boniface Pawasa, Ulimboka Mwakingwe, Emmanuel Gabriel, Juma Kaseja, Yahya Akilimali, Said Maulid ‘SMG’, Suleiman Matola na wengine wengi.