AVEVA (KUSHOTO) AKIWA NA BAADHI YA WADAU, BENNY KISAKA NA JUMA PINTO AMBAYE NI MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO TANZANIA (TASWA). |
Mmoja wa watakaowania nafasi ya Rais mpya wa klabu ya Simba, Evans Aveva atachukua fomu kesho.
Taarifa zinasema Aveva ataongozana na rafiki zake kadhaa ambao watamsindikiza katika makao makuu ya Simba kuchukua fomu hizo.
Aveva ni kati ya wanachama wa Simba wanaounda kundi la Friends of Simba na amewahi kuliongoza kwa mafanikio.
Ni kati ya wanaopewa nafasi kubwa kuitwaa nafasi hiyo baada ya Zacharia Hans Pope kukosa nafasi ya kushiriki.