Mtangazaji maarufu wa vipindi katika runinga, Maimartha Jesse amegeuka kivutio dukani kwake kwa kujiremba na kuvaa mawigi tofautitofauti ili kuwavuta wateja.
Mbali na urembo, mtangazaji huyo amekuwa akiwaita majina wateja wake majina ambayo hutumika siku hizi kuita wapenzi kama vile baby, mwenyewe anadai kuwa ni lugha ya kuwakaribisha na kuwakarimu wateja.