Staa wa kike anayetikisa kwenye tasnia ya filamu na muziki, Snura Mushi a.k.a Majanga anadaiwa kuwa ni mmoja wa mastaa wa kike wenye ujuzi mkubwa kimahaba kiasi cha kuwapagawisha mno wanaume anaokuwa nao katika mahusiano.Chanzo chetu cha habari ambacho kiko karibu na staa huyo kilieleza kuwa Snura huwa na tabia ya kupandisha mzuka wa jukwaani awapo kwenye sita kwa sita na wakati mwingine huweza hata kuvunja kitanda endapo akiamua kufanya hivyo.....
"Unajua Snura anaasili ya kizaramo, Amefundwa kila aina ya mafunzo ya kuwa na mwanaume.Mimi ni rafiki yangu kwa kipindi kirefu, yaani tokea niwe karibu naye wanaume aliowahi kuwa nao wamemsifu kuwa anaweza mambo tena si kitoto", Kilieleza chanzo hicho
Inadaiwa kwamba asilimia kubwa ya mastaa wa kike huwa hawapendi kujishughulisha wawapo faragha kutokana na ustaa wao,lakini taarifa za Snura zimekuwa tofauti....
Mwandishi wetu alimtafuta Snura ambaye baada ya kumuuliza aliangua kicheko:
"Sasa utamu wa ngoma si ni lazima uicheze? Huwezi kujua hivi hivi.Hayo mambo ni mazito sana naona kwangu ni ngumu kuyazungumzia kwa sababu najiandaa kuolewa. Ila kwa mwanamke hasa wa taipu yangu ni lazima ujue kumpetipeti mume.
"Hilo halinipi shida sana sababu nimekamilika kila idara.Mbele ya watu kibao shughuli inakuwa pevu jukwaani sembuse chumbani wawili tu?" Alisema staa huyo anayefunika Tanzania na ngoma yake ya Nimevurugwa