$ 0 0 Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dengue: Unayohitaji Kujua Dengue ni ugonjwa unaoleta homa kwa muda wa siku 2 hadi 7 na huambatana na dalili zifuatazo: - Kuumwa kwa macho. - Kuumwa kwa kichwa. - Maumivu ya misuli na viungo. - Kutokwa na damu (katika fizi au pua). - Kukwaruzika kwa urahisi. Huduma ya nyumbani kwa homa ya Dengue ni: - Pata vinywaji kwa wingi mfano maji, juisi au chai. - Tumia dawa za maumivu kupunguza homa. - Usitumie dawa ya "Aspirin" ama "Ibuprofen" Nenda hospitali haraka unapoona moja ya dalili za tahadhari. Dalili za tahadhari za kuangalia baada ya homa kuondoka: - Maumivu makali ya tumbo. - Kutapika mfululizo. - Kutokwa damu. - Ngozi kupauka na kuwa baridi. - Kudhoofika kwa mwili, usingizi mzito. - Kizunguzungu, kuzimia. - Kupumua kwa shida.