Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

YULE KIONGOZI MTATA WA CHADEMA ALIYESIMAMISHWA AFUNGUKA TENA LIVE!!

$
0
0

 
"Kwa nini tunakuwa wepesi kudanganyika kiasi hiki? Yaani leo AG amesema, tena kirahisi kabisa kwamba ZZK hana majina ya mabilionea wetu walioweka mapesa huko nje na watu ghafla ahaaaa, huyu jamaa kumbe ni mwongo? Swali la kwanza kabla ya kumshabikia AG ni je kuna wenzetu wenye mabilioni katika akaunti za nje? Kama hivyo hizo hela ziliendaje? Hakuna watu wenye hizo akaunti? Na kama wapo nani mwenye jukumu la kuwajua-ni serikali, mbunge au raia yeyote?
Ripoti iliyotolewa mwaka jana na Benki Kuu ya Uswisi (Swiss National Bank) ilionyesha kwamba watazania wana fedha zipatazo dola za kiamerikani 196 millioni, lakini hawakutaja majina ya wenye akaunti hizo. Kwa hiyo kwamba kuna watanzania walioficha mahela huko nje sio hisia, ni jambo la kweli. Swali ni nani mwenye jukumu la kuwataja hao watu? Kwa nini serikali inakwepa wajibu?

Tuachane na siasa nyepesi nyepesi. Tuanze kuuliza maswali angalau marahisi kwa kuanzia. Tunajaribu kujenga hoja kwamba kila chuo kikuu hapa nchini kianze kufundisha somo la critical thinking kwa kila mwanafunzi!"
Like· · ·  · 11 hours ago near Dar es Salam·

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>