MKONGWE wa filamu za Kibongo, Sabrina Rupia ‘Cathy’ ameibuka na kusema kuwa katika tasnia ya filamu hawezi kutokea msanii wa kufanana na aliyekuwa msanii na muongozaji wa filamu, Adam Kuambiana.
Akistorisha na gazeti hili, Cathy alisema yeye na Kuambiana walikuwa wakiishi maisha ya kutaniana, kila walipokuwa wakizungumza alikuwa akimtania mambo mengi na siku moja kabla ya kifo chake alizungumza naye kwenye simu kwa muda mrefu tofauti na siku nyingine huku akimtania sana.
“Nahisi kama Kuambiana alikuwa anajua anakufa maana siku moja kabla ya kifo chake tuliongea kwa muda mrefu sana kwenye simu ukweli naumia sana najiuliza kwa nini niliongea naye hivyo ila ndiyo hivyo tena Mungu amempenda zaidi na ninaamini kwamba hakuna msanii anayeweza kufanana na Kuambiana kwa ucheshi na utendaji kazi wake,” alisema Cathy.