Kyela. Mmoja wa watoto pacha waliozaliwa wakiwa wameungana na kutenganishwa kwa upasuaji nchini India, hali yake ni mbaya na utumbo wake mkubwa sasa umetoka nje.
Mtoto huyo Eliud Mwakyusa na mwenzake Elikana walizaliwa Februari 20, 2013, Kyela, Mbeya wakiwa wameungana kiunoni na Serikali iliwapeleka India ambako walitenganishwa.
Walirejea Februari, mwaka huu na kusherehekea siku yao ya kuzaliwa wakiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili walikofikia baada ya kutoka India katika hafla iliyoandaliwa na gazeti hili.
Hata hivyo, siku chache baada ya watoto hao kurejea kijijini kwao Kasumulu maarufu kwa jina la Juakali, Kyela, afya ya Eliud ilianza kubadilika baada ya sehemu kubwa ya utumbo wake mpana kuanza kutokeza nje.
Utumbo wa mtoto huyo umetoka nje kupitia tundu lililoachwa na madaktari jirani na kitovu chake kwa ajili ya kutolea haja kubwa.
Wakizungumza na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki nyumbani kwao, wazazi wa watoto hao, Grace Joel na Eric Mwakyusa walisema tatizo la Eliud lilianza mwezi mmoja uliopita.SOMA ZAIDI HAPA>>>>>