Wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wanaolipiwa na Bodi ya Mikopo wakimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo hicho aliyekuwa akiongea nao.
Makamu Mkuu wa Chuo akijaribu kuwatuliza wanachuo hao kwa kuwaahidi kushughulikia suala lao.
Viti vikiwa vimetawanywa baada ya vurugu zilizosababishwa na mgomo huo.
WANAFUNZI wanaolipiwa na Bodi ya Mikopo katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kilichopo Mabibo Mwisho jijini Dar, jana wamegoma na kufanya vurugu wakidai kucheleweshewa fedha zao za mkopo. Mgomo huo umeanza majira ya saa 6 na nusu mchana ambapo polisi waliingilia kati kutuliza ghasia zilizokuwa zinaendelea chuoni hapo. Mpaka mtoa habari hii anaondoka eneo la tukio, bado wanachuo walikuwa wakisubiri majibu ya uongozi wa chuo hicho.