Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MGONJWA WA SARATANI ALIYETELEKEZWA AFARIKI DUNIA

$
0
0

Mgonjwa wa saratani ambaye alidai kupewa tiba feki za mionzi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (OCRI), Pendo Shoo amefariki dunia  juzi wilayani Karatu akiwa safarini kuelekea Kirua Vunjo, Kilimanjaro kwa wazazi wake.
Mdogo wa Pendo, Digna Shoo, alisema dada yake alifariki juzi, saa nne usiku wakati wanafamilia wakimfanya maombi.
“Alianza kubadilika ghafla wakati tukiwa katikati ya maombi, alilegea na mgongo wake ukawa kama unapinda hivi, tukamshika na tukamweka kitandani,” alisema.
 Digna alisema kwamba baada ya kumweka kitandani  mtumishi wa Mungu aliyekuwa nyumbani hapo alimwombea na hazikupita dakika nyingi akakata roho. Alisema Pendo alikwenda Karatu akitokea Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita, kipindi ambacho hali yake ilikuwa imeshatetereka sana kiasi cha kushindwa kutembea mpaka apate msaada wa mtu karibu.
“Wakati tunatoka Dar es Salaam kuja Karatu, hali yake ilikuwa imeshakuwa mbaya, alikuwa hawezi kutembea bila kumpa ‘support’ (msaada) alikuwa anapepesuka,” alisema Digna.SOMA ZAIDI >>>>>>>

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>