Lori la mafuta aina ya Scania lenye namba za usajiri T772 BAZ limetumbukiakwenye mtaro eneo la Kihonda barabara kuu ya Morogoro Dodoma baada ya dereva wa Lori hilo kushuka na kuliacha gari hilo bila kulizima na kuwafukuza wezi waliokuwa juu ya tenk la gari hilo wakishusha mizigo.
" Dereva wa Lori hili alipofika pale kwenye tuta alishuhudia pikipiki ikiwasha taa na kuzima aliamua kuongeza umakini na kubani kwamba mmoja wa abiri aliyekuwa kwenye pikipiki hiyo alipanda juu ya Tenk na kushusha maboksi ya Oil ndipo dereva huyo aliposhuka akajisahau kuvuta 'endbrack'hivyo wakati akiwafukuza wezi hao huku Lori hilo lililokuwa kwenye mtelemko lilitembea bila dereva na kuingia kwenye mtaro
Dereva wa Lori hilo Bw ldd Hoza alipohojiwa alisema alikuwa akisafirisha mafuta ya petroli kutoka Dar es salaama kueleka Dodoma na kwamba alipofika kwenye daraja la Kihonda alipunguza mwendo kwa lengo la kulipanda tuta lililokuwa eneo hilo la daraja.
Kwa kawaida dereva unapopunguza mwendo ni lazima uangalie kwenye kioo nyuma yako kuna nini hivyo nilipoangalia niliona dereva wa pikipiki akiwasha taa na kuzima nilipochunguza zaidi nikaona mtu yuko juu ya Tenk akishusha maboksi ya Oil nikashuka na kumfukuza kwakuwa eneo hili ni la mtelemko gari hili lilitembea lenyewe na kuingia kwenye mtaro na wezi hao walifanikiwa kuondoka na boksi moja la oil kwa kutumia pikipiki yao"alisema Dereva huyo ambaye mpaka muda huu huyo hapo eneo la Tukio
Picha Kwa Hisani ya Shekidele Blog