Ukweli sakata la kukamatwa walioitwa house boys na girls nyumbani kwa Lwakatare
Wandugu,LUDOVICK ALIKUWA MOJA YA MAAFISA WANDANI WA CHADEMA NA AMEFANYA KAZI KWA UKARIBU SANA NA LWAKATARE KWENYE KITENGO CHA INTELEJENSIA YA CHADEMA HADI HAPO ALIPOAMUA KUACHANA NA KAZI HIYO
Siku chache zilizopita, kulikuwa na taarifa zilizoshtua kuhusu kukamatwa walioitwa house maids wa Lwakatare kimara nyumbani kwake. taarifa iliyotolewa haraka na kurugenzi ya habari ya chadema jamii forums ilisema kuwa ulikuwa ni mwendelezo wa serikali ya CCM kubambikizia chadema kesi, hasa baada ya kushindwa kuhusu ile kesi ya ugaidi.
Nilisumbuliwa sana binafsi na
mashabiki wa chadema wengine wakivamia nyumbani kwangu na kutaka kunijeruhi kwa kuuza vijana hawa wa Lwakatare kwa polisi na CCM. hata hivyo ukweli ulikuwa tofauti kabisa na kile kurugenzi yz habari ya chadema ilikuwa inatangaza.
Ni kuwa Nyumbani kwa Lwakatare kuna bar ya kuuza pombe. na hapo dada anayeishi kwa lwakatare ni mhudumu wa bar hiyo na vijana wawili wanaishi hapo na ni ndugu wa msichana huyo mhudumu wa bar. sasa yaonekana kuna kijana anatuhumiwa kuwa mwizi wa magari Arusha, na akiwa Dar huwa anakunywa kwenye bar hiyo karibu na nyumbani kwa lwakatare na amechukua namba ya dada muuza baa ambaye ni ndugu wa lwakatare.
Katika uchunguzi na kufatilia nyendo za jamaa huyo, ndipo ilionekana amekuwa anawasiliana na dada huyo muuza bar na huyo dada anaonekana anawasiliana na ndugu zake hao wawili. kwa hiyo kukamatwa kwao ilikuwa ni jambo la kawaida kabisa la kiuchunguzi na ilipobaiika kuwa mawasiliano yao hayakuwa na uhusiano wowote wa kihalifu waliachiwa bila masharti yoyote.
Lakini kurugenzi ya habari tena katika vyombo vya habari ilishaanza propaganda kuwa vijana hao wanabambikizwa kesi na CCM. HII INA MAANA WATU AMBAO NI WANA CHADEMA AU WANA UHUSIANO NA VIONGOZI WA CHADEMA WASICHUNGUZWE PALE INAPOONEKANA KUNA UMUHIMU WA KUFANYA HIVYO KWA VYOMBO VYA DOLA?
na je kwa nini kurugenzi ya habari iliamua kuingilia uchunguzi wa polisi na kutoa habari za uongo? hii ni tabia mbaya na isiyokuwa na mantiki. kwani kurugenzi ya habari inataka kuaminisha watu kuwa watu katika chadema hawawezi kutenda jinai au hawawezi kuchunguzwa na vyombo vya dola bali wanabambikizwa tu kesi jambo ambalo siyo kweli.
Na nimejaribu kutafuta mahali ambapo kurugenzi ya habari chadema imesahihisha uongo wake baada ya watu hao kuachiwa sijaona. kwa nini chadema inapenda kuishi kwa uongo?
Chanzo:HAPA