Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

MSANII BONGO MOVIES ATANGAZA KUTAKA MUME MWENYE PESA NYINGI NA SI MBABAISHAJI

$
0
0
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Kibongo Husna Chobis ‘Awena’ amesema kuwa baada ya kurudi katika biashara zake nje ya nchi yupo tayari kuolewa lakini kwa mwanaume mwenye fedha za kutosha na siyo mbabaishaji.
Akifafanua zaidi, msanii huyo amesema hawezi kuolewa na mwanaume ambaye hawezi hata kumiliki Bajaji.
Pia, amedai kwamba mwanaume mwenye fedha za kubadilisha mboga hana mpango nao.
“Kuzaliwa katika familia ya kimaskini ni bahati mbaya, lakini kuchagua mume maskini ni uzembe na hustahili kusamehewa,” alisema.

Aidha aliongeza kuwa kutembea kwake amejifunza mambo mengi na kuona mastaa wa Ulaya huwa wanaolewa kwa maslahi.

Mwigizaji huyo aliyejizolea umaarufu katika Filamu ya Ndase, alisema moja ya matatizo ya ndoa za Kitanzania au Kiafrika ni kukosea katika uchaguzi na kuingia katika uhusiano.

“Wengi huishia kupotezeana muda kisha kutengana kutokana na kuwa uzembe wa kukosea katika uchaguzi wa mume au mke,” alisema.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles