AIJAKAA poa! Staa wa sinema za Kibongo, salome Ndumbagwe Misayo ‘Thea’ na rafiki yake wa kitambo ambaye pia ni mwigizaji, Vanitha Omary wamepishana kauli na kuchambana vilivyo msibani kwa komediani mkongwe, Said Ngamba ‘Mzee Small’.
Mwigizaji wa Bongo muvi, Vanitha Omary akitabasamu.
Ishu hiyo iliibuka mara baada ya Thea kumtuhumu Vanitha kumuita mume wake mnafiki kwa kitendo cha kulikacha Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) na kujiunga na Bongo Movie Unity ndipo ‘kikanuka’.Baada ya ugomvi kutulia, mwanahabari wetu aliwatafuta wawili hao, kila mmoja akaongea lake.