ZIKIWA zimepita wiki kadhaa tangu kuripotiwa kupatanishwa kwa mastaa wawili katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja, taarifa zisizo na shaka zilizotua kwenye meza ya Ijumaa Wikienda zinaeleza kwamba upatanisho huo haukusaidia chochote na sasa bifu jipya limeibuka kati yao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kilichoomba hifadhi ya jina lake, zoezi la upatanishi kati ya mastaa hao lililofanyika kwenye msiba wa dairekta wa filamu za Kibongo, George Tyson, Mbezi Beach jijini Dar lilikuwa sawa na kazi bure.
“Hakuna yeyote kati yao aliyekuwa na nia ya dhati ya kumaliza tofauti zilizokuwepo, walikubali kupatana kwa sababu ya heshima ya waliokuwa wanawapatanisha lakini kiukweli ilikuwa ni sawa na danganya toto, bifu limelipuka upya,” kilisema chanzo hicho ambacho ni rafiki wa karibu wa mastaa hao wakubwa mjini.