Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa kuna baadhi ya rafiki zake walifurahia alipokamatwa na mzigo wa matirio yaliyodhaniwa ni unga Mei, mwaka jana nchini Afrika Kusini.
Akizungumza mitandaoni, mrembo huyo ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake Johannesburg, Sauzi alisema: “Kuna marafiki zangu wengine walikuwa wanapenda nikae ndani, si unajua sisi hatupendani?
“Mimi naweza nikakupenda wewe ukiwa na kitu, lakini mimi nikipungukiwa na kitu fulani huwezi kuwa rafiki yangu tena sababu Agness kakwama kitu fulani, kwa hiyo atakuwaje rafiki yangu?
“Wengine walikuwa wakiongea Agness alikuwa anaringa bora aende jela.”
“Wengine walikuwa wakiongea Agness alikuwa anaringa bora aende jela.”