Pichani ni Bw.Joseph Magessa aliyetuhumiwa hivi karibuni na tukio la Nyoka aina ya Chatu.
SAKATA la kukutwa na chatu eneo la sakina katika nyumba ya Joseph Magessa limechukua sura mpya baada ya mhusika kuhojiwa na mtandao wa jamiiblog huu kuhusiana na tukio hilo.Aidha chatu huyo ambaye alikutwa nyumbani kwa mmiliki huyo hivi karibuni imeelezwa tuhuma hizo sio za kweli bali ni njama za kumuharibia tu na tukio hilo ni la kutengenezwa na watu kwa lengo la kumchafulia jina lake.Magessa alisema kuwa ,ameshangazwa sana na tukio hilo kwani lilipotokea alikuwa safarini yeye na mke wake , ndipo alipopigiwa simu kuhusiana na tukio hilo na kuwataarifu huyo chatu auawe.
.
Pia, amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu zilizolenga kumchafua na kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.
Pia, amedai kuwa hizo zinaweza kuwa njama za watu zilizolenga kumchafua na kwamba, suala hilo amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye ukweli.
Aliongeza kuwa, yeye hajawahi kuwa mshirikina wala mke wake bali wanachojua wao ni kuwa wanamtumikia Mungu na yeye pekee ndiye ajuaye kila jambo na kuwa mambo yote hayo yaliyotokea amemwachia Mungu ndiye atakayejibu.Magessa alifafanua kuwa, ameshangazwa sana na taarifa mbalimbali ambazo zimekuwa zikizushwa kwenye vyombo vya habari pamoja na mitandao juu ya tukio hilo ila yeye amenyamaza kimya na amemwachia Mungu kwani ndiye ajuaye kila kitu.INAENDELEA HAPA >>>>>>.