Mnenguaji wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis akionyesha sehemu alikopigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi.
MNENGUAJI wa Kundi la Kanga Moko, Zawia Hamis ambaye usiku wa Jumatano iliyopita alipigwa risasi mbili mwilini na mtu aliyedaiwa ni askari polisi, ameweka undani wa sakata hilo.
Akizungumza na gazeti hili juzi nyumbani kwake Mwananyamala jijini Dar, majeruhi huyo alisema tukio hilo lilijiri maeneo ya Mwananyamala- Kisiwani karibu na Ofisi za Chama cha Wananchi (Cuf) na kuongeza kuwa, kisa ni kubishana na askari huyo aliyetaka kuzimwa kwa matarumbeta kutoka kwenye kikundi chao kilichokuwa kikipita eneo hilo.
“Sisi tulikuwa tukipita na matarumbeta, askari wakatusimamisha na kutuamuru tuyazime kisha kutaka kutukamata watupeleke kituoni eti serikali imekataza. “Tuliwaambia mbona ni mapema sana kwani ilikuwa saa kumi alasiri na Kova alisema ngoma za Kanga Moko, Kigodoro na nyingine zisipigwe usiku. Pia tuliwaambia tulichokuwa tukikifanya si ngoma hasa, ni matarumbeta tunapita kuwaalika watu kuwa leo kuna shughuli sehemu.INAENDELEA HAPA>>>>>>>>