*************
Serengeti:Ni jambo la kawaida kuwaona wanaume wilayani Serengeti wakiongozana na wake ama watoto wao siku za minada, kwenda kuuza mifugo ili wanunue mahitaji yao, lakini mapato hudhibitiwa na wanaume.
Mara baada ya mauzo na kununua mahitaji,wanawake na watoto hulazimika kurudi nyumbani huku wanaume wakibaki wakistarehe ,huzitumia siku ,ni nadra mwanaume kuwahi kurudi nyumbani .
Mei 19, Rhoda Nyangi Mtatiro (24) mkazi wa Kitongoji cha Kenyana kijiji cha Masangura kata ya Ring’wani wilayani Serengeti, licha ya ujauzito wa miezi sita alionao alikubali kuongozana na mumewe Wang’enyi Sabai(30) kutoka kijijini kwao hadi Rung’abure umbali wa kilometa zaidi ya 15 kwa mguu.
Huku wakiswaga kondoo wanne walifanikiwa kufika mnadani na kuwauza wakajipatia fedha za mahitaji hakujua kuwa kuna balaa lingemkuta siku hiyo, pamoja na kuswaga na kutembea umbali mrefu na ujauzito wake hakuambulia kitu zaidi ya kipigo ambacho leo hajui hatima ya maisha yake.
Licha ya kufanikiwa kuuza kondoo wote aliambulia Sh 2,000 kwa ajili ya kununua nguo za mtoto wao mmoja kati ya wanne walionao anayesoma darasa la kwanza shule ya Msingi Geitasamo, iliyoko hapo Rung’abure ambako ni kwao na Rhoda.inaendelea >>>>>>>>>>