Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa kwa sasa hatakubali tena kusumbuliwa na wanaohoji juu ya maisha yake mapya ya wokovu.
Staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’.
Akizungumza na paparazi wetu, Mainda alisema mwanzoni alikuwa anapata shida sana kuishi na watu kwani yeye kama msanii kila anachofanya watu wanachukulia ndivyo sivyo na hata katika wokovu pia wanahoji kama atauweza kitu ambacho anaamini hatotetereka.
“Nimejifunza vitu vingi sana kutokana na ustaa wangu, watu wengi wananiangalia kwa jicho linginewanataka kuona je Mainda ana mabadiliko gani baada ya kuokoka? Ninapoteleza kama mwanadamu utasikia watu wanasema mimi si mlokole, siwajali kwa sasa,’’ alisema Mainda.