Muimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka THT, Amini Mwinyimkuu ameamua kufunga ndoa baada ya ile ishu aliyoifungua mwenyewe juu ya kumpa mimba mke wa mtu pasipo kufahamu kuwa ni mali ya mwanaume mwenzake na baadae kuanza pata vitisho toka kwa mume wa mwanadada aliyebeba mimba hiyo.
Amini amefunga ndoa hiyo jana June 22 na msanii Farida Bashir maarufu kama Nancy Vana aliyeimba ‘Kantangaze’.