Quantcast
Channel: Blogu ya Wananchi
Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

LULU AKANUSHA KUSHIRIKISHWA NA MAPACHA KATIKA WIMBO WAO MPYA

$
0
0
Kundi la Mapacha linaloundwa na Kulwa na Dotto limeachia wimbo wao mpya unaoitwa Times For The Money ambao wamedai kumshirikisha Elizabeth Michael aka Lulu. 
Katika hali isiyo ya kawaida, Elizabeth Michael aka Lulu amekana katu kutowahi kushirikishwa na wasanii hao na kwamba huenda umefanyika muujia. 
Kupitia Instagram, Lulu ameandika: 
 Mwe mwe mwe...!Mbona mnaninyasanyasa...'in Senga's voice'
 I swear sina idea na Huku kushirikishwa....au kuna Elizabeth Michael'Lulu' mwingine!???? 
Dah...hebu mliosikia hyo nyimbo labda mniambieMana nashirikishwa ki miujiza jmn.
Kwa maelezo ya Mapacha wao walikuta mdundo wa wimbo huo studio ukiwa na sauti ya kike kwenye chorus na wakaipenda, baada ya kufanya kazi ndipo Tudd Thomas akawaambia kuwa sauti hiyo ameifanya Lulu. 
So, Tudd aliwafunga kwenye gunia Mapacha?! Na Je, kwa nini Mapacha hawakumtafuta Lulu kumshukuru kwa chorus kabla ya kutangaza chochote?..Tunza majibu yako vizuri.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 32622

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>