Akiwa angani: Obama akitazama mechi ya mwisho ya Marekani dhidi ya Ujerumani akiwa kwenye ndege yake.
RAIS wa Marekani, Barack Obama ameonesha jinsi gani kombe la dunia ni muhimu kwa taifa lake baada ya kuamua katazama mchezo wa mwisho wa kundi G dhidi ya Ujerumani akiwa kwenye ndege yake binafsi.
Obama alikuwa anasafiri kwa ndege kutoka Maryland kwenda Minnesota wakati Marekani ikicheza mchezo muhimu na alihakikisha hakosi mchezo huo kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye luninga iliyopo kwenye ndege yake.
Mashabiki wa timu ya taifa ya Marekani walishangilia timu yao wakiwa kote Marekani na Brazil.
Kikosi cha Mjerumani, Jurgen Klinsmann kilipoteza mechi kwa goli la Thomas Muller, lakini kimefuzu hatua ya mtoano kwa wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Ureno.
Klinsmann alichapisha barua ya kuomba sapoti kutoka kwa mashabiki wa Marekani na viongozi kwa ujumla.
Ruksa: Gavana wa New York , Andrew Cuomo alijibu maombi ya Klinsmann kwenye mtandao wa Twita.