January 2014 balozi wa Tanzania nchini China aliongea kwenye na kusema Watanzania wanaoshikiliwa kwenye magereza mbalimbali nchini humo hawazidi 200 lakini idadi yao ni zaidi ya 100 ambapo asilimia kubwa kilichowapeleka huko ni kesi za dawa za kulevya.
Ilipofika March 25 2014 katibu mkuu wa wizara ya mambo ya nje John Haule alitaja idadi ya Watanzania waliokamatwa kwa ishu ya dawa za kulevya China na nikamkariri akisema ‘Katika Magereza ya China mpaka February 2014, tumepewa taarifa na mamlaka za China kwamba wapo Magerezani Watanzania 177 ambapo 15 kati yao wamehukumiwa kunyongwa kutokana na biashara hiyo ya dawa lakini niseme tu wenzetu wa Serikali ya China wanatuthamini sana kama sisi tunavyowathamini’
Alimalizia kwa kusema ‘wenzetu wa China wanathamini zaidi uhusiano wetu na ndiyo maana hata wale wachache Watanzania waliohukumiwa kunyongwa hawajanyongwa mpaka leo na hatutegemei kama watanyongwa, yani sanasana watafungwa kifungo cha maisha gerezani’
Sasa taarifa iliyotoka June 25 2014 kutoka tume ya kudhibiti dawa za kulevya imesema wamekamata zaidi ya tani 2.3 za dawa za kulevya na vilevile vigogo 12 wa biashara hiyo wamekamatwa.
Kingine ni kwamba kwa mwaka huu wa 2014 pekee idadi ya Watanzania waliofungwa nchini Brazil kwa kesi za dawa za kulevya ni 113 ambapo taarifa hiyo haikufafanua zaidi kuhusu hukumu zao na mengine yanayoambatana.