Mjumbe wa Bunge la Katiba Mh. Paul Makonda akifungua Tawi jipya la wakereketwa ka Steve Nyerere Bwawani Kinondoni jana kabla ya kumsimika Steve Nyerere kuwa Kamanda mpya wa UVCCM wa tawi hilo. |
Mh. Paul Makonda + Le Big Show |
Steve Nyerere akivalishwa nguo za Ukamandana Mama yake mzazi jana!! |
Super Designer Asya Idarious |
Mh. Paul Makonda Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la mabadiliko ya Katiba Komred Paul C. Makonda leo hii Tarehe 27/6/2014 amefanya kazi kubwa ndani ya Mkoa wa Dsm...Wilaya Kinondoni...kata ya Mwananyamala...Tawi la bwawani kwa kufungua mashina ya wakereketwa (Wajasiliamali) na Kumsimika Kamanda wa Vijana wa Tawi la Bwawani Ndg STEVEN MANGERE aka Steve Nyerere. Katika kusherehesha sherehe hizo za Kumsimika kamanda huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bongo Movie Tanzania wasanii mbalimbali wa bongo freva na wasanii wa filamu walitoa burudani ya kufa mtu... Hakika sherehe zilifana kupita kiasi. Baadhi ya wasanii na waigizaji wa filamu waliokuwepo hapo ni...JB ... RICHIE RICH... BABA HAJI...CHIKOKA...JOHARI...KIM...ELIETY...SANDRA...ODAMA...Rose Ndauka...MSAGASUMU....MAKOMANDOO...na wengineo kibao. Hakika leo ilikuwa burudani tosha ndani ya maeneo ya Bwawani Mwananyamala. Lakini pia nimeamini wasanii wote wenye akili timamu wapo CCM isipokuwa wale waliopungukiwa na utimamu tu wakina Afande sele bange mtu ndio wapo Chagadema. Safari ya mafanikio ya mwaka 2014 tumeshaianza DSM...tutarudisha Majimbo...Kata...na hata mitaa ukiwemo mtaa wa Bwawani ambapo Kamanda Steve Nyerere ameahidi kuurudisha CCM Mwaka huu wa uchaguzi. Sambamba na Mgeni Rasmi pia kulikuwepo na viongozi mbali mbali wa CCM na UVCCM....Ambao ni Mjumbe wa Baraza kuu la UVCCM Taifa.. William J. Malecela aka Le Mutuz Baharia...Mjumbe wa NEC Asha Baraka...Katibu wa UVCCM Mkoa DSM Kidando...Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Mka wa DSM Komred Saady Khimji... Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kinondoni...Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi Wilaya Kinondoni ndg Omar Omary Bomba...na viongozi mbalimbali wa Kata na Tawi.... Bila kumsaau Mwanamitindo Maarufu ndani na nje ya Tanzania Dada ye Asia Idarous naye alikuwepo. Kwa mwenendo huu CCM Mkoa DSM haikamatiki. Vivaa CCM Vivaaa....' Aluuuuuutaaaaaaa ' |