Deogratius Mongela na Chande Abdallah
SIKU chache baada ya kuvunjika kwa ndoa ya Khadija Shaibu ‘Dida’, aliyekuwa mumewe, Mtangazaji wa TV1, Ezden Jumanne ameibuka na kutoa sababu kuu tatu za kutengena kwao, Risasi Mchanganyiko linakupa zaidi.
Akizungumza na waandishi wetu katika nyumba aliyohamia kwa sasa, Kijitonyama, Dar, Ezden alisema mgogoro kati yake na Dida ulianza zamani ambapo Dida alikuwa na tabia ya kurudi usiku mnene, Ezden alidai kadiri siku zilivyozidi kusonga mbele, tabia hiyo ilizidi kuonekana ingawa alikuwa akimuonya mara kwa mara.
BIG BROTHER NDIYO TATIZO
Pamoja na sababu hizo, Ezden aliitaja sababu kuu iliyoanza kuzua mgogoro uliosababisha kuvunjika kwa ndoa hiyo ni Shindano la Big Brother Africa linalotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Alisema siku moja mtalaka wake huyo alimweleza kuwa kuna rafiki yake aliyemtaja kwa jina la Furaha amempa mchongo wa kuwa mgeni staa (celebrity guest) ndani ya Jumba la Big Brother na kumuomba ampe ridhaa ya kwenda huko.endelea hapa>>>>>>>>>>>