Gurumo (kulia) akipagawisha huku akisindikizwa na Hafsa Kazinja na Hussein Jumbe (kushoto).
Hussein Jumbe na mcharaza gitaa maarufu, Miraj Shakashia 'Shakazulu' wakinogesha mambo.
Sehemu ya mashabiki.
Mmoja wa mashabiki akimtunza Gurumo baada ya kumkoleza.
Gurumo akishindilia noti mfukoni.
Shabiki huyu inaonekana alikumbushwa mbali sana.
Mashabiki hawa baada ya kunogewa walivamia jukwaa.
Mpiga tarumbeta mwenye makeke, Roman Mng'ande 'Romario' akipagawisha mashabiki.
Mashabiki wakiserebuka na mwanamuziki wa Msondo, Hassan Moshi.
Mzee Makasi (kulia) akiburudisha mashabiki. Kushoto ni mcharaza gitaa mahiri, Hamza Kalala 'Komandoo'.
Katika tamasha hilo, Gurumo alitangaza kuwa warithi wa kazi yake ya kuimba ni hawa, Hussein Jumbe (kulia), Edo Sanga (kushoto) na Juma Katundu.
WADAU wa burudani nchini usiku wa kuamkia leo walifurika kwenye Viwanja vya TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam kwenye tamasha la kustaafu muziki gwiji wa dansi hapa nchini, Maalim Muhidini Gurumo. Katika tamasha hilo, wakongwe kadhaa wa muziki walimsindikiza mwenzao kutoa burudani.GPL