Vijana wa kike na wa kiume walionaswa wakifanya vitendo viovu uchochoroni. MAJANGA! Timu ya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers inayodili ya maeneo korofi kwa uovu, imewanasa vijana wa kike na kiume wakifanya vitendo vichafu vichochoroni, maeneo ya Mbagala-Zakheem, Dar. Awali, OFM ilipokea malalamiko kutoka kwa wakazi wa maeneo hayo juu ya vijana hao kufanya ngono vichochoroni na kusababisha kuzagaa kwa maboksi ya mipira ya kiume (kondom) maeneo hayo kutokana na kutupwa hovyo baada ya kutumika.
Baadhi ya akina dada walionaswa na OFM katika zoezi hilo. Baada ya kufanya utafiti na kuona hali halisi, OFM wakishirikiana na askari kutoka kituo kidogo cha polisi cha Mbagala-Kizuiani, walitinga katika eneo hilo saa nane usiku hivi karibuni na kuwanasa laivu machangu kadhaa na wateja wao katika banda moja la mama ntilie.
Kijana akijificha sura baada ya kutiwa nguvuni. OFM ilizungumza na mmoja wa machangu hao ambaye alidai kuwa kilichompeleka mjini kutafuta maisha akitokea mkoani Mara ambapo mtu aliyempokea ambaye ni changu mwenzake (hakuwepo eneo la tukio) alimleta hapo na kumfundisha biashara hiyo.
Watuhumiwa wakipandishwa kwenye gari la polisi. “Haka kabiashara kananisaidia na mimi nimeweza kupanga chumba na kununua nguo na chakula, mimi na machangu wenzangu tunacheza upatu kama njia ya kujiendeleza kimaisha, nisingeweza kama nisingefanya biashara hii,” alisema changu huyo pasipo kutaja jina. Mbali na eneo hilo, OFM ilishuhudia vibanda vingine vinavyotumiwa na machangu hao na wateja wao kufanya ngono na kujionea kondom na makasha mengi yaliyotumika kwa siku hiyo. Mwishoni, machangu hao na wateja wao walichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kisha mapema siku iliyofuata walipandisha Mahakama ya Jiji la Dar kusomewa mashitaka ya uze