MASANJA MKANDAMIZAJI APEWA MAKAVU
KWAKO, Emmanuel Mgaya ‘Masanja’. Naamini u mzima na unaendelea vyema na majukumu yako ya kila siku. Kwa upande wangu nipo sawa, nakimbizana na maisha.
Nina machache ya kukushauri kuhusiana na maisha yako kama staa ambaye kwa sasa umetangaza kuokoka. Kwa maneno mengine ni kwamba, umeondoka kwenye utaifa, upo mikononi mwa Muumba wako.Nimekufahamu kwa kitambo kidogo. Kwangu mimi, wewe ni mmoja wa mastaa wa ukweli katika uchekeshaji Bongo.
Mwenye kipaji cha hali ya juu na unayejua unachokifanya.
Tatizo ni kwamba, nashangazwa na aina ya maisha yako baada ya kutangaza kuokoka. Ninavyojua mimi, kuokoka ni kuachana na maisha ya awali ambayo (pengine) yalikuwa hayampendezi Mola na kugeukia katika maisha safi.Niliposikia umeokoka nilifurahi kuona kuwa umeelekea sehemu sahihi zaidi kiimani. Lakini moyoni nilikuwa na shaka kidogo maana wapo wasanii wengi kwenye uigizaji ambao walitangaza kuokoka lakini baadaye wakaonekana kwenye njia zao za awali.
Ukiachana na waigizaji, pia kuna wasanii wa Bongo Fleva ambao nao waliingia kwenye ulokole na mara wakaamua kurudia maisha yao ya awali.Baadaye nikasikia kuwa unasomea Uchungaji (ingawa inaelezwa kuwa ni Uinjilisti), hapo sikuwa na shaka tena na wokovu wako. Niliamini kwa mtu ambaye ameamua kuingia kwenye kufundisha wengine njia iliyo sahihi hawezi kudanganya kuwa ameokoka.Siyo kama naingilia maisha yako au nakukosoa kwenye suala la imani yako. Uzuri ni kwamba, nami ninaamini katika imani yako, hivyo sioni tatizo kukushauri.Tatizo lipo kwenye staili yako ya maisha. Ni kweli kwamba umeokoka, lakini itawezekana vipi usuke mabutu kichwani? Maandiko yanaeleza wazi kuwa, wanaoamini ni barua inayosomeka kwa watu wote.
Je, watu watasoma nini kupitia mabutu? Unaweza kusema kuwa, imani ya mtu iko moyoni, hapo sitakubaliana na wewe, maana kinachoonekana nje, kinawakilisha kilichomo ndani.Vipi kama kanisa zima, wanaume wataingia wamesuka? Nafikiri si jambo sahihi. Watu watapata shaka na wokovu wako, tena mchunga kondoo. Wengine wanaweza kuona wokovu si jambo ‘serious’. Kwamba mtu anaweza kuingia na akaendelea na mambo yake yaleyale, jambo ambalo si la kweli.
Wokovu ni pamoja na mwonekano wa nje. Mavazi, mitindo ya nywele n.k.Jambo jingine ambalo limenishangaza ni namna unavyoingiza komedi kwenye mambo yanayohusu dini.Usahihi wa kufanya utani kwenye vichekesho huku ukitaja jina la Mungu unatokea wapi? Masanja tumezuiwa kufanya mzaha au kulitaja bure Jina la Mungu wetu.
Nakushauri kama ni kweli umeamua kuokoka, badilika lakini kama unahisi bado unatamani maisha ya kawaida na kujichanganya, chagua moja ili jamii isikutafsiri tofauti.Ni uamuzi wako kufuata au kuacha hapahapa, lakini la muhimu ni kwamba, nitakuwa nimeshakushauri. Ubarikiwe sana mpendwa!

- AnonymousJuly 3, 2014 at 7:08 AMHta mi nakuunga mkono mtoa ushauri uchague kusuka ama kunyoka unaambiwa Masanja huwez kuwa vuguvuvu chagua moja kaka kuwa moto ama Baridi..mf nyimbo zako za Injili mi binafsi hazinibariki kwa kuwa umeweka mzaha mwingi hii inapelekea wasikilizaj kuona kitu cha Mungu ni kawaida sana .....Jiangalie BroReply
- AnonymousJuly 3, 2014 at 8:09 AMWHO are you to judge??? Hauna cha kufanya maishani mwako utafute ya mwenzio?? Pole mwenzio yuleeeeee na bila shaka namba umeisoma ndo mana mapovu yanakutoka!Reply
- AnonymousJuly 3, 2014 at 9:32 AMkila mtu na maisha yake..yeye masanja mbona ni mtu mzima na anajitambua...shauri ndugu zako na wauza unga na serikali ...na tanesco..acha uoga wewe!!...Reply
- Yani ukitaka kipindi chako kikose kiki mjini basi kipekeje Tbc1 ndoninachokiona sasa kwa Zecomed, kukiwa na ufunguzi cjui wa nini nini kipindi hamna, ,rais akienda kumpokea nani cjui eapoti kipindi kinahaitishwa, bunge vilevile yaani ni shida, ndomqna show nyingi zipo EatV. Iiizi redio za Tanu izi taabu kwelikweli. By the way mie jayika ma comedian wooote bado Joti anabaki kuwa namba moja kwangu.Reply
- AnonymousJuly 3, 2014 at 11:17 AMHivi Masanja ana mabutu or hajachana nywele? Hyu the so called mlokole ndiyo wale wale kwa nje watakatifu lakini mioyoni mwao ni wabaya kuliko chatu. Ndiyo wale wakikukuta umesimama na mlokole atamsalimia hyo mlokole na kukuacha wewe kama vile ni jini fulani. Ndiyo kuna mavazi ambayo yanakwaza watu kama vimini, kata k na mengine ya hayo. But mabutu! Sielewi maana sioni ni jinsi gani mabutu ya Masanja yatawashawishi wanaomuona kuingia majaribuni kama vile kimini na kata k.Reply
- AnonymousJuly 3, 2014 at 11:18 AMMhh mimi hapa nina shid akidogo na Sinta katika kupost hizi post zako. najua kama Administrator unapokuwa unapost unauwezo wa kuedit layout au muonekano wa post yako na unaweza ukaview kabla hata hujaipost ili kuangalia kama imekaa sawa au ni madudu. sasa hizi post zako nyingi ziku hizi unavyopost inakuwa shida maana zinakata baadhi ya maneno tunashindwa kusoma. jirekebishe kwenye hilo na kama hulijui uliza basi wajuaji.Reply
- AnonymousJuly 3, 2014 at 11:19 AMWokovu ni wa mtu na mungu wake.., maisha yake hayakuhusuuu wafateee mapadri na mashekh, na wachungaji wanaozini...., ukae ukijua kuokoka ni process si swala la kuchange mara hiyo hiyo, alafu aliekuambia wenye vipara ndo wataingia mbingujni na wenye mabutuu wataenda jehanamu nani?. Hujui maana ya kuokaa weweee ndo yale ya zamani eti kuoka unatakiwa uwe mchafu mchafu au mchungaji atembee kwa mguuu asiwe na gari. Utabaki kumjudge hapo mwenzako uhusiano wake na mungu wake anaujuaa, we unaconclude kwa mabutuuu umelobaaaa step kwanzaaa kuwaa na akili timamu ndo upost mambo ya imani ya mtu.Reply
- Mungu pekee ndo a najua ana chokifanya masanja ni sahii au cio tek tym yako for busnes an leave masanja only God can judge himReply
- AnonymousJuly 3, 2014 at 7:10 PMnyie wengine mnapiga debe tu lakini mhusika ujumbe umemfikia.PSALM 1:1Reply
- AnonymousJuly 4, 2014 at 6:20 AMkuhusu imani, ni yeye na Mungu wake wala hakuna sababu ya kumhukumu kwa hilo. ila mimi naona hapendezi kuwa hivyo ili awe smart basi atengeneze nywele zake vizuri tu. kwani siku hizi kuna mitindo mingi tu ya kukata nywele ya kisasa itakayomfanya aonekana wa heshimia, wa kisasa na nadhifu.