Neymar akiwa amelala chini baada ya kupata majeruhi ya mgongo dakika tatu kabla ya mechi kumalizika.
NYOTA wa Brazil, Neymar, ataikosa mechi ya nusu fainali baina ya wenyeji dhidi ya Ujerumani jumanne ijayo, hii ni kwa mujibu wa kocha, Luiz Felipe Scolari.
Taifa mwenyeji limefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya ushindi wa mabao 2-1 mjini Fortaleza, lakini nyota wake alitolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika na amekimbizwa hospitali baada ya mechi kumalizika kutokana na kupata majeruhi ya mgongo.
Neymar amekuwa akijikaza kuimarika katika mechi zote za Brazil kutokana na majeruhi ya goti, lakini alifaulu kuanza katika mechi zote.
Hapa machela: Neymar akitolewa nje ya uwanja kwa machela, huku akiwaacha mashabiki na taifa zima likiwa katika hofu kubwa.
Juan Zuniga akimgonga Neymar mgongoni kwa goti
Mtu chini: Mshambuliaji wa Barcelona akianguka chini baada ya kugongwa mgongoni na sasa yupo katika wasiwasi mkubwa wa kucheza nusu fainali.
Ndio mwisho wake? Neymar akiwa amebebwa kwa machela na kuna wasiwasi kuwa inaweza kuwa mwisho wa kucheza kombe la dunia mwaka huu.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona amefunga mabao manne katika fainali za mwaka huu, lakini alishindwa kuongeza dhidi ya Colombia kabla ya kutolewa nje kwa machela dakika tatu kabla ya mechi kumalizika.
Kocha wa Brazil Luiz Felipe Soclari alisema: "Sidhani kama ataweza kucheza mechi ijayo".
"Amekimbizwa hospitali binafsi na madaktari kwasababu aligongwa na goti katika mgongo wake".
" Alikuwa analia kwa maumivu. Haitakuwa rahisi kwake kuimarika kwa kuzingatia ukweli kwamba ni majeruhi ya mgongo na maumivu aliyonayo ni makubwa. Acha tuwe na matumaini kuwa kila kitu kinakwenda vizuri".